Lugha Nyingine
GDP ya Eneo Kuu la Ghuba la China yakadiriwa kufikia yuan trilioni 15 katika mwaka 2025

Picha hii iliyopigwa Desemba 8, 2022 ikionyesha mandhari ya Eneo la Ushirikiano wa Sekta ya Huduma za Kisasa la Qianhai, Shenzhen na Hong Kong katika mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Liang Xu)
GUANGZHOU - Eneo Kuu la Ghuba la Guangdong-Hong Kong-Macao (GBA) la China linasukuma mbele mafungamano, ambapo utoaji wa jumla wa uchumi wa eneo hilo unakadiriwa kuzidi yuan trilioni 15 (dola za Marekani takribani trilioni 2.15) katika mwaka 2025, mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la Mkoa wa Guangdong umesema.
Eneo kuu hilo la ghuba linaunganisha mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao pamoja na miji tisa ya mkoa wa Guangdong China, ikiwemo miji ya Guangzhou, Shenzhen na Zhuhai. Eneo hilo linazidi kuwa na mawasiliano mengi katika sekta mbalimbali kutokana na usafiri wa haraka na mzunguko mzuri zaidi wa kiuchumi wa kuvuka mipaka.
Habari zilizotolewa kwenye mkutano huo wa mwaka zimesema, muunganisho wa miundombinu halisi umeongeza kasi katika miaka ya hivi karibuni ambapo njia za reli za kuunganisha miji zimebadilika kuwa mfumo wa mtandao, zikipeleka urefu wa jumla wa reli kufikia kilomita zaidi ya 4,000, huku njia za abiria wa majini zinazovuka mipaka zikipanuka hadi kufikia njia 17.
Imeeleza kwenye mkutano huo wa mwaka wa bunge kuwa muunganisho wa kitaasisi pia unaanza kuwa dhahiri, na hivi sasa watu wanaweza kupata huduma 198 za serikali za kuvuka mipaka katika sehemu mbalimbali ndani ya eneo hilo la ghuba. Mamlaka zimeanzisha vigezo 267 vya Eneo Kuu la Ghuba la Guangdong-Hong Kong-Macao (GBA) na kutoa idhini 308 za eneo kuu hilo la ghuba.
Katika eneo hilo kwa hivi sasa kumekuwa na vituo 84 vya uvumbuzi na ujasiriamali kwa vijana kutoka Hong Kong na Macao, vikiwa vimevutia miradi zaidi ya 7,000.
Hali ya mwelekeo huu imeonesha nguvu halisi iliyo pana zaidi ya uchumi wa Mkoa wa Guangdong. Kwa mujibu wa ripoti ya kazi ya serikali ya mkoa, ambayo imetolewa kwenye mkutano huo wa mwaka wa bunge, mkoa huo wa kusini mwa China umechukua nafasi ya kwanza nchini China katika GDP ya jumla kwa mwaka wa 37 mfululizo katika mwaka 2025.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



