Lugha Nyingine
Bunge la Ulaya laahirisha uamuzi juu ya makubaliano ya biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani
Picha hii iliyopigwa Juni 6, 2024 ikionyesha mwonekano wa nje ya Bunge la Ulaya jijini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
BRUSSELS - Bunge la Ulaya limeahirisha uamuzi wake hadi wiki ijayo, uamuzi ambao unahusu kama lianzishe upya kazi au la kuhusu makubaliano ya biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, baada ya kusitisha kwa muda mchakato wake wa kuidhinisha uamuzi huu wiki iliyopita kwa kuwa kupinga shinikizo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuichukua Greenland na ushuru wa tishio dhidi ya washirika wa Ulaya.
Bernd Lange, mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya Kimataifa ya Bunge la Ulaya, amesema jana Jumatatu kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba hakuna uamuzi uliotolewa jana Jumatatu wa kuanzisha tena utaratibu wa kawaida wa utungaji wa sheria kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, na timu ya mazungumzo ya Bunge itakutana Februari 4 ili kutathmini upya hali ya mambo.
Januari 21, Bunge la Ulaya liliamua kusitisha kwa muda idhini ya makubaliano ya biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani kutokana na ushuru wa tishio kutoka Marekani unaohusu na Greenland.
Hali ya wasiwasi ilipungua baadaye wakati Washington ilipotangaza kwamba "makubaliano ya kimfumo" yalikuwa yamefikiwa juu ya masuala husika ya Greenland na kwamba ushuru huo uliokuwa umetishiwa kwa nchi nane za Ulaya utasitishwa kwa muda.
Kutokana na makubaliano ya biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani yaliyofikiwa Julai mwaka jana, Umoja huo unatakiwa kuondoa ushuru kwa bidhaa zote za viwanda vya Marekani na kuweka mgao wa ushuru kwa aina mbalimbali za mazao ya kilimo ya Marekani yanayoingia katika soko la Umoja wa Ulaya.
Kwa kulingana na hayo, Washington inatakiwa kuweka kikomo cha ushuru cha asilimia 15 kwa bidhaa nyingi za Umoja wa Ulaya zinazouzwa nchini Marekani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



