Timu ya wanawake ya Uganda kushiriki kwa mara ya kwanza kwenye Michuano ya ITTF ya Ubingwa ya Timu za Tenisi ya Mezani Duniani 2026

(CRI Online) Januari 27, 2026

Timu ya wanawake ya Tenisi ya Mezani ya Uganda itashiriki kwa mara ya kwanza kwenye Michuano ya Ubingwa ya Timu za Tenisi ya Mezani Duniani ya Shirikisho la Tenisi ya Mezani Duniani (ITTF) ya Mwaka 2026.

Kwenye droo ya michuano hiyo iliyofanywa jana Jumatatu na ITTF, timu hiyo ya Uganda imepangwa kwenye Kundi 6 pamoja na India, Ukraine na Rwanda.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Aprili hadi tarehe 10 Mei mwaka 2026 kwenye Ukumbi wa OVO Wembley mjini London.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha