Namibia kuharakisha sheria za uhalifu wa mtandaoni, kupanua muunganisho wa 5G vijijini

(CRI Online) Januari 27, 2026

Waziri wa Teknolojia ya Kupashana Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Namibia Emma Theofelus amesema Nambia itaharakisha sheria ya kupambana na uhalifu wa mtandaoni na ulinzi wa data, kupanua muunganisho wa kidijitali vijijini na kuimarisha usimamizi wa kampuni za umma za TEHAMA za nchi hiyo.

Akizungumza jana Jumatatu kwenye mkutano wa kufungua mwaka wa mazungumzo kati ya watumishi, waziri huyo amesema mashauriano na wadau kuhusu rasimu ya mswada wa sheria hiyo yataanza tena Februari 2.

“Sheria inayopendekezwa inatarajiwa kushughulikia uhalifu unaowezeshwa na teknolojia, ikiwemo unyanyasaji wa mtandaoni, ufuatiliaji haramu wa mtandaoni, matumizi mabaya ya picha na kutumia kwa unyonyaji picha feki, huku mkazo mahsusi ukiwekwa kwenye ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia” ameongeza.

Emma amesema mswada huo uko tayari kuwasilishwa tena kwenye kamati ya baraza la mawaziri inayohusika na utungaji wa sheria kabla ya kuwasilishwa bungeni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha