Lugha Nyingine
Ndege za kivita za J-10 za timu ya sarakasi za ndege angani ya PLA zawasili Singapore kushiriki kwenye maonyesho

Ndege za Timu ya Sarakasi za Ndege Angani ya Bayi ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) zikiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Changi wa Singapore, Januari 27, 2026. (Picha na Zhu Jianghai/Xinhua)
SINGAPORE - Ndege saba za kivita za J-10 kutoka Timu ya Sarakasi za Ndege Angani ya Bayi ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) zimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Changi wa Singapore jana Jumanne ili kufanya maandalizi kwa kushiriki kwenye Maonyesho ya 10 ya Ndege Angani ya Singapore, yaliyopangwa kufanyika Februari 3-8.
Msemaji wa Kikosi cha Anga cha PLA Xie Peng amesema hii ni mara ya 13 kwa timu hiyo kufanya maonesho ya urukaji wa ndege nje ya nchi, na pia ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kurudi kwenye Maonyesho ya Ndege Angani ya Singapore tangu maonyesho hayo ya saba yaliyofanyika mwezi wa Februari mwaka 2020. Amesema ndege hizo zimeambatana na ndege ya tanki ya YY-20A, ambayo iliwezesha ndege hizo kujazwa mafuta wakati wa safari hiyo ya kuelekea Singapore.
Xie amesema timu hiyo imepangwa kufanya maonyesho kadhaa ya urukaji wa ndege angani pamoja na ndege kutoka nchi nyingine zinazoshiriki kwenye maonesho. Ameongeza kuwa uwanja wa kupaa na kutua kwa ndege na eneo la kufanya maonyesho hayo vipo kwenye sehemu tofauti, na maonyesho yamepangwa kufanyika pia juu ya bahari.
Timu hiyo ya sarakasi za ndege angani iliyoanzishwa miaka 64 iliyopita, imefanya maonesho ya urukaji wa ndege angani kwa zaidi ya mara 800 kwa jumbe zaidi ya 800 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 180.

Ndege za Timu ya Sarakasi za Ndege Angani ya Bayi ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) zikiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Changi wa Singapore, Januari 27, 2026. (Picha na Zhu Jianghai/Xinhua)

Ndege ya Timu ya Sarakasi za Ndege Angani ya Bayi ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Changi wa Singapore, Januari 27, 2026. (Picha na Zhu Jianghai/Xinhua)

Ndege za Timu ya Sarakasi za Ndege Angani ya Bayi ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) zikionekana huko Singapore, Januari 27, 2026. (Picha na Zhu Jianghai/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



