Lugha Nyingine
Spika wa Bunge la Umma la China afanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Senegal

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Malick Ndiaye, Spika wa Bunge la Senegal, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, Januari 27, 2026. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Senegal Malick Ndiaye mjini Beijing jana Jumanne.
Zhao, amesema China inapenda kushirikiana na Senegal kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, pamoja na Mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kuendelea kuimarisha maudhui ya ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya China na Senegal, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika ya hali zote yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Amesema kwamba Senegal imesisitiza hadharani kwamba inafuata bila kuyumbayumba kanuni ya kuwepo kwa China moja, na China inapongeza sana hilo.
"China itaendelea kuiunga mkono Senegal katika kufuata njia huru na ya kujitegemea ya maendeleo," ameongeza.
"Nchi zote mbili zinapaswa kupanua ushirikiano wa sifa bora na wa kunufaishana, na kuchunguza nguvu zao bora za ushirikiano katika maendeleo ya viwanda na kilimo cha kisasa, biashara na uwekezaji, nishati mpya, na uchumi wa kidijitali," Zhao amesema.
Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuzidisha mawasiliano katika maeneo kama vile utamaduni, elimu, vyombo vya habari, vijana, huduma za afya, michezo na ngazi za serikali za mitaa ili kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya China na Senegal, na kati ya China na Afrika.
Zhao ametoa wito wa uratibu na ushirikiano wa karibu ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Umoja wa Kati ya Mabunge Duniani ili kuongeza sauti na uwakilishi wa nchi za Kusini mwa Dunia.
Kwa upande wake Ndiaye amesema kwamba Senegal inafuata bila kuyumbayumba kanuni ya kuwepo kwa China moja, inathamini kwa kiwango cha juu mapendekezo manne ya kimataifa yaliyotolewa na China, na inapenda kuendelea kuhimiza maendeleo ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na China, na kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
"Bunge la Senegal lina nia ya kuzidisha mawasiliano na ushirikiano na Bunge la Umma la China, na kubeba jukumu la kivitendo katika kuhimiza ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili," Ndiaye amesema.

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Malick Ndiaye, Spika wa Bunge la Senegal, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, Januari 27, 2026. (Xinhua/Zhang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



