Lugha Nyingine
Zimbabwe yaripoti mlipuko wa kipindupindu kutokana na mafuriko
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 28, 2026
Idara ya Ulinzi wa Raia (DCP) ya Zimbabwe imesema Zimbabwe imerekodi mlipuko wa kipindupindu uliosababisha kifo cha mtu mmoja katika Wilaya ya Rushinga, Jimbo la kati la Mashonaland.
Idara hiyo imesema katika taarifa yake Jumatatu wiki hii kuwa hadi kufikia Januari 22 watu watatu walioambukizwa ugonjwa huo na kifo kimoja vimerekodiwa katika wilaya hiyo iliyo karibu na Msumbiji.
Idara hiyo pia imesema kituo cha matibabu ya kipindupindu kimeanzishwa katika eneo hilo, huku mifumo ya ufuatiliaji ikiwa imeimarishwa.
Wizara ya afya na huduma kwa watoto ya Zimbabwe tarehe 22 mwezi huu ilitahadharisha umma juu ya hatari inayoongezeka ya kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na mvua kubwa na mafuriko katika sehemu nyingi za nchi hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



