Lugha Nyingine
Programu ya mafunzo ya TEHAMA kwa vijana ya kampuni ya Huawei yaanza rasmi mjini Nairobi
Programu ya mafunzo kwa vijana 21 wa Kenya waliochaguliwa kushiriki kwenye mashindano ya teknolojia ya kupashana habari na mawasiliano (TEHAMA) yanayofadhiliwa na kampuni ya Huawei ya China kwa mwaka 2025-2026 imeanza rasmi jana Jumanne mjini Nairobi.
Washiriki hao walioteuliwa kutoka kwenye orodha ya maombi takribani 3,000 kutoka vyuo vikuu na vituo vya mafunzo ya ufundi kote nchini Kenya, watapewa mafunzo, malezi ya kitaaluma na kujifunza kutoka kwa wenzao kwa lengo la kuongeza ujuzi wao wa kidijitali.
Meneja mafunzo wa akademia ya mafunzo ya TEHAMA wa kampuni ya Huawei Bw. Michael Kamau, amesema programu hiyo ya mafunzo inakusudia kuwapa washiriki ujuzi wa kidijitali wa hali ya juu, ili kuwaandaa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya TEHAMA ya kampuni hiyo na kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa ushindani kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



