Ufunguaji mlango wahimiza ongezeko kubwa la wageni wanaoingia China na kuimarisha maingiliano kati ya watu (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2026
Ufunguaji mlango wahimiza ongezeko kubwa la wageni wanaoingia China na kuimarisha maingiliano kati ya watu
Watalii wa Italia wakitembelea Hifadhi ya Taifa ya Misitu ya Zhangjiajie katika Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Januari 2, 2026. (Picha na Wu Yongbing/Xinhua)

Zikichochewa na sera zinazopanuka za China za msamaha wa visa, safari za watalii wa kigeni wanaoingia China ziliongezeka maradufu mwaka 2025, huku idadi ya watalii walioingia kupitia msamaha huo wa visa ikipanda kwa asilimia 49.5 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia hadi kufikia watalii karibu milioni 30.1, takwimu rasmi zilizotolewa jana Jumatano na Mamlaka ya Kitaifa ya Uhamiaji ya China zinaonesha.

Mamlaka hiyo imesema jana Jumatano kwamba wageni wa kimataifa walivuka mipaka kwa zaidi ya mara milioni 82 kwa jumla, ikiwakilisha ongezeko la asilimia 26.4 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia wa 2024.

Kwa sasa, China inatoa msamaha wa visa kwa raia wa nchi 76. Aidha, wasafiri kutoka nchi 55 wanaweza kufurahia sera ya msamaha wa visa wa kuingia na kukaa China kwa saa 240 katika sehemu 65 tofauti za kuingia ndani ya China.

Mbali na safari za kutembelea kwa muda mfupi, ufunguaji mlango wa China unajenga jumuiya yenye nguvu hai ya wakazi wa kimataifa. Wasomi, wanafunzi, na wataalamu zaidi wanachagua kuishi na kufanya kazi nchini China, hali ambayo inaongeza kwa kina uhusiano wa kati ya watu. China, ambayo ina mambo na maeneo mengi ya kujionea au kutembelea kutalii na hata vingine vingi, inaendelea kuvutia watu duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha