China yapanua huduma za kusafirisha wanyama vipenzi kwa reli ya mwendo-kasi kwa pilika za usafiri wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2026
China yapanua huduma za kusafirisha wanyama vipenzi kwa reli ya mwendo-kasi kwa pilika za usafiri wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi
Mhudumu akiangalia hali ya mnyama kipenzi kupitia kreti mjini Lanzhou, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China, Februari 1, 2026. (Xinhua/Chen Bin)

Huku msimu wa pilika za usafiri wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China zikiwadia, Stesheni ya Magharibi ya Reli ya Lanzhou katika Mji wa Lanzhou, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China imekaribisha abiria kadhaa wanyama vipenzi wa binadamu. Abiria hawa vipenzi hufuatiliwa na kutunzwa kimaalum na wahudumu wa treni, wakisafiri ndani ya masanduku maalum ya kusafirisha wanyama vipenzi yaliyo na mifumo ya ufuatiliaji inayotumia akili mnemba.

Tangu Januari 28, mamlaka za reli za China zimeongeza zaidi idadi ya stesheni za reli za mwendo-kasi zenye huduma za kusafirisha wanyama vipenzi. Abiria wanaweza kuweka oda za nafasi mtandaoni kupitia programu ya 12306 au programu ndogo ya mtandao wa kijamii wa WeChat, na kufanya usafiri wa wanyama vipenzi kuwa rahisi zaidi wakati wa kipindi cha Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha