Lugha Nyingine
Treni za mwendo-kasi za sehemu mbalimbali China zajiandaa kwa ajili ya pilika zijazo za usafiri wa wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi (9)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2026
![]() |
| Picha iliyopigwa Februari 1, 2026 ikionyesha treni za mwendo-kasi zikijiandaa kutoa huduma, Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China. (Picha na Zhang Wen/Xinhua) |
Treni za mwendo-kasi katika sehemu mbalimbali nchini China zinajiandaa kwa pilika zijazo za usafiri wakati wa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, zinazojulikana pia kwa jina la chunyun, ambazo zitaanza leo Februari 2 katika mwaka huu wa 2026.
Kila mwaka wakati wapilika nyingi za usafiri, mamilioni ya watu wanaofanya kazi, wanaosoma au wanaoishi mbali na maskani zao hurudi nyumbani kwa ajili ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya jadi ya China, na kuleta wimbi kubwa zaidi la mwaka la usafiri wa watu duniani.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




