Viwanda vya uundaji meli vya China vyaendelea kuongoza duniani katika mwaka 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 03, 2026
Viwanda vya uundaji meli vya China vyaendelea kuongoza duniani katika mwaka 2025
Picha iliyopigwa Januari 3, 2026 ikionyesha eneo la kazi ya kuunda meli la Kampuni ya Kiwanda cha Meli cha Duchang katika Mji wa Jiujiang, Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China. (Picha na Fu Jianbin/Xinhua)

Viwanda vya uundaji meli vya China vimedumisha nafasi kubwa zaidi kwenye soko duniani kutokana na viashiria vitatu vikuu vyake vya mwaka wa 16 kwa mfululizo katika mwaka 2025, takwimu zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Upashanaji wa Habari ya China siku ya Jumapili zinaonesha.

Katika mwaka 2025 uliopita, uundaji wa meli wa jumla wa China ulifikia tani milioni 53.69 za uzito (DWT) ongezeko lake lilifikia asilimia 11.4 ikilinganishwa na mwaka wa 2024 na kuchukua asilimia 56.1 ya jumla duniani.

Na oda mpya za viwanda hivyo vya China zilifikia DWT milioni 107.82 mwaka jana, ikichukua asilimia 69 ya sehemu ya soko la dunia.

Na hadi kufikia mwisho wa Desemba 2025, oda hodhi za viwanda hivyo vya China zilikuwa DWT milioni 274.42, ongezeko lake lilifikia asilimia 31.5 kuliko mwaka 2024 . Kiasi hicho kilichukua asilimia 66.8 ya sehemu ya soko la dunia.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha