Lugha Nyingine
Tamasha la Shehuo lavutia hadhira kwa sanaa ya jadi katika Mji wa Urumqi, China (4)
![]() |
| Watu wakifurahia tamasha la Shehuo mjini Urumqi, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Februari 26, 2026. (Xinhua/Ding Lei) |
Tamasha la Shehuo limefanyika mjini Urumqi, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China jana Alhamisi. Tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na watumbuizaji zaidi ya 2,000, lilihusisha kanivali yenye jukwaa lililopambwa na maonyesho mbalimbali ya Shehuo, aina ya sanaa ya jadi ya China.
Shehuo, onyesho lenye umaarufu mkubwa ambalo limekuwa likiheshimiwa na kuthaminiwa kwa muda mrefu katika maeneo ya vijijini kote China, linatokana na shughuli za kale za matambiko za kuomba mavuno mazuri miaka takribani 2,000 iliyopita.
Baadaye, baada ya maonyesho ya densi na uimbaji kuingizwa ndani yake, hatua kwa hatua Shehuo lilibadilika na kuwa desturi ya jadi inayotumbuizwa kwenye sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi na sikukuu ya Taa za Jadi, likiaminika kuwa linaondoa bahati mbaya na kuleta mwanzo mpya katika mwaka mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




