Treni ya mwendo-pole yatumika kama “Soko linalohamahama” kwa wanakijiji Kusini Magharibi mwa China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2026
Treni ya mwendo-pole yatumika kama “Soko linalohamahama” kwa wanakijiji Kusini Magharibi mwa China
Wafanyakazi wa reli wakisaidia wanakijiji kushuka kwenye treni baada ya treni No. 5630 kuwasili kwenye Stesheni ya Reli ya Tongzi, Zunyi, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Februari 25, 2026. (Picha na Wang Bo/Xinhua)

Treni No. 5629/5630 inayopita kwenye sehemu za milimani zenye hali nguvu ya kijioglafia ni "treni ya mwendo-pole" inayounganisha Mji Zunyi mkoani Guizhou, kusini-magharibi mwa China, na Mji wa Chongqing kusini-magharibi mwa China.

Tangu ianze kutoa huduma miaka 33 iliyopita, treni hiyo si tu inafuata kanuni za kutoza nauli za pesa chache na kusimama kwenye kila kituo, ikileta urahisi wa usafiri wa kila siku na usafirishaji wa mazao ya kilimo wa watu wanaoishi kwenye sehemu zilizoko kando za njia ya reli hiyo, bali pia imeweka sehemu maalum kwa wakulima ndani ya mabehewa, ili kusaidia wakulima wa mboga za majani kuhifadhi na kuuza mazao yao ya kilimo.

Treni hii imekuwa "soko linalohamahama" kwa watu wa huko, na pia imesaidia mazao ya kilimo ya sehemu hizo kufikia kwenye masoko mengi zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha