Fundi mwandamizi wa treni afuatilia zaidi kujiendeleza kwa vipaji vijana wa kazi ya ufundi (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2026
Fundi mwandamizi wa treni afuatilia zaidi kujiendeleza kwa vipaji vijana wa kazi ya ufundi
Dong Hongtao (mbele, kushoto) akimfundisha kijana wa studio ya wataalamu ya daraja la kitaifa anayoiongoza mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Januari 14, 2026. (Xinhua/Li Yibo)

Dong Hongtao ni fundi wa treni za mwendo-kasi wa Kampuni ya Kundi la Reli la Xi'an la China, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Tangu ajiunge na kazi ya matengenezo ya treni za mwendo-kasi (EMU) mwaka 2007, Dong amekuwa akiongoza timu yake kufanyia matengenezo seti zaidi ya 120,000 za treni hizo na kushughulikia hitilafu zaidi ya 3,000.

Ameshapewa hataza tatu za uvumbuzi za kitaifa na hataza 31 za mifumo ya matumizi. Dong pia amejitolea kurithisha ujuzi wa kiufundi, na anasaidia kuwaandaa vipaji na watu wenye ujuzi kwa kupitia studio ya wataalamu wa daraja la kitaifa inayoendeshwa naye.

Dong amekuwa fundi mwandamizi hatua kwa hatua kuanzia kazi ya mfanyakazi wa kawaida, hivyo anaelewa changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa mstari wa mbele katika kujiendeleza kwao. Ameona kuwa wafanyakazi hao kwa kawaida wana uzoefu mwingi lakini hawana ujuzi wa kinadharia. Hivyo amefanya juhudi za kushiriki katika hatua mbalimbali za kuwasaidia kuongeza ujuzi wa ufundi wao na kutambua vipaji vijana na kuwasaidia kukuza ubunifu wao.

Kuhusu kuhudhuria kwenye mkutano wa mwaka huu wa Bunge la Umma la 14 la China, Dong amesema ataendelea kufuatilia hali ya kujiendeleza kwa vipaji wa kazi ya ufundi, kuweka mkazo katika kusukuma mbele utekelezaji wa mfumo wa kutathimini cheo cha kazi mpya za kitaaluma, ambao unahusisha cheo cha kazi nane za kitaalamu ambazo zimeongezwa tatu kuliko mfumo wa zamani wa ngazi ya tano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha