Tamasha la Shehuo lafanyika Urumqi, China (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2026
Tamasha la Shehuo lafanyika Urumqi, China

Tarehe 26, Februari, tamasha la pili la Shehuo la Urumqi "Kupiga ngoma ya mikononi na kucheza dansi ya dragon" lilifanyika kwenye kituo cha utamaduni cha Urumqi, Xinjiang, China. Tamasha hilo, ambalo ni sehemu ya mwisho ya maonesho ya Shehuo ya mwaka huu ya Urumqi, lilifanyika kwenye njia yenye urefu wa kilomita 3, na kushirikisha timu 16 za wasanii wazuri kutoka mji wa Urumqi na timu kutoka mikoa na miji mingine iliyoalikwa. Magari tisa yenye mapambo yaliyoonesha mitindo mbalimbali na mada tofauti yalishiriki kwa shangwe kwenye tamasha hilo, na idadi ya washiriki ilizidi 2,000.

Katika shughuli hiyo, magari ya mapambo yaliyokuwa kama majukwaa yalihamahama, na maonesho ya dansi ya dragon na simba, maonesho ya kupanda farasi na maonesho mengine ya kijadi yalifanywa juu ya majukwaa hayo, yakivutia sana wakazi kusimama, kutazama na kupiga picha ya kumbukumbu.

Shughuli hiyo iliwawezesha wakazi kujionea mvuto wa mila na desturi na pia kuongeza uhai wa mji wa kurithisha na kukuza utamaduni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha