Lugha Nyingine
Mjumbe wa Bunge la Umma la China atoa wito wa maendeleo ya "AI pamoja na viwanda" (4)
![]() |
| Zhang Fan (kulia) akikagua kituo cha utafiti cha Kundi la Zana na Vifaa vya Umeme la China mjini Shanghai, mashariki mwa China, Januari 27, 2026. (Xinhua/Liu Ying) |
Zhang Fan ni naibu meneja mkuu wa Kundi la Zana na Vifaa vya Umeme la China ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Zhang anaona kuwa "teknolojia ya AI pamoja na viwanda vya utengenezaji bidhaa" vitaweza kutimizwa kwa kupitia kufanya mpango wa jumla kuhusu utendaji wa pande mbalimbali na kwenye ngazi tofauti.
Mwaka jana, Zhang aliwasilisha pendekezo juu ya kuzidisha kwa kina mafungamano ya viwanda vya utengenezaji bidhaa na teknolojia ya AI na kuhimiza maendeleo ya uvumbuzi yenye sifa bora. Pendekezo lake hilo limetiliwa maanani sana.
Mwezi Januari 2026, idara nane za China ikiwemo Wizara ya Viwanda na Upashanaji wa Habari ya China kwa pamoja zilitoa mpango unaoelezea matarajio makubwa ya kusukuma kwa kina mafungamano ya kina zaidi ya teknolojia ya AI na viwanda vya utengenezaji bidhaa, kukuza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuongeza uwezo kwa pande zote ili kupanua nafasi za maendeleo ya viwanda vya aina mpya.
Zhang amesema kwamba ataendelea kufuatilia zaidi masuala kuhusu vizuizi vya kunufaika pamoja na data katika viwanda vya utengenezaji bidhaa kwa kutegemea teknolojia ya AI pamoja na maarifa yaliyopatikana kwa mafanikio katika viwanda vya kuongoza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




