Masomo mbalimbali yawasaidia wanafunzi kujenga uwezo wa kupata ufundi wa shughuli za vito za kisasa mkoani Shandong, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2026
Masomo mbalimbali yawasaidia wanafunzi kujenga uwezo wa kupata ufundi wa shughuli za vito za kisasa mkoani Shandong, China
Mwalimu (katikati) akielekeza wanafunzi kupima na kuthibitisha bidhaa kwenye kituo cha usimamizi wa ubora katika Chuo kikuu cha Elimu ya Awali cha Qingdao katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Machi 31, 2026. (Xinhua/Li Ziheng)

Katika miaka ya hivi karibuni, chuo cha vito katika Chuo kikuu cha Elimu ya Awali cha Qingdao cha Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China kimehusisha mchakato halisi wa shughuli za vito katika masomo yake kwa kupitia kutumia kituo cha mafunzo na jukwaa la uzoefu wa uzalishaji katika chuo hiki.

Darasani, wanafunzi wanasoma nadharia kuhusu vito na kupata ufundi wa kutambua vito, kufanya matengenezo, ukataji na ung'arishaji wa vito. Pia wanaweza kupata ujuzi mbalimbali ukiwemo wa usanifu wa vito wa AIGC, uundaji wa modeli za 3D, na utangazaji wa moja kwa moja wa biashara ya mtandaoni. Aidha, wanafunzi wanaweza kushiriki katika michakato ya uzalishaji na usimamizi wa ubora wa bidhaa za vito viwandani ili kupata ujuzi unaohitajiwa katika shughuli husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha