Siku ya Mashua ya Qintong yaadhimishwa katika Mji wa Taizhou, Mkoa wa Jiangsu, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2026
Siku ya Mashua ya Qintong yaadhimishwa katika Mji wa Taizhou, Mkoa wa Jiangsu, China
Picha iliyopigwa Aprili 6, 2026 ikionesha mashua zikishiriki kwenye mashindano ya kuadhimisha Siku ya Mashua ya Qintong yaliyofanyika kwenye Bustani ya Kitaifa ya Ardhi Oevu ya Qinhu katika mji wa Qintong wa Mji wa Taizhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China (Picha na Tang Dehong/Xinhua)

Siku hiyo ya Mashua iliwekwa katika Enzi ya Song ya Kusini ya China ya zama za kale (1127-1279), inasemekana kuwa siku hiyo iliwekwa kwa kukumbuka mababu na mashujaa wa zama za kale.

Shughuli ya kuadhimisha siku hiyo imefanyika jana Jumatatu, ambapo mamia ya mashua zenye wapigao kasia kwa mwanzi zaidi ya 10,000 zilikusanyika katika eneo hilo na kushiriki kwenye mashindano ya mwendo kasi. Siku hiyo ya Mashua iliyoendelea kuadhimishwa kwa mamia ya miaka imeorodheshwa kuwa moja ya urithi wa kitaifa wa utamaduni usioshikika wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha