China yarekodi safari milioni 135 za kufanya utalii wa ndani wakati wa mapumziko ya Siku ya Qingming (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2026
China yarekodi safari milioni 135 za kufanya utalii wa ndani wakati wa mapumziko ya Siku ya Qingming
Watalii wakiwa wamepanda rafti za mianzi wakifurahia mandhari kwenye mto katika Wilaya ya Xuan'en, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Aprili 4, 2026. (Picha na Song Wen/Xinhua)

Takwimu zilizotolewa jana Jumanne na wizara ya utamaduni na utalii ya China zimeonesha kuwa, safari za watu kwenda kufanya utalii katika sehemu mbalimbali nchini zilifikia milioni 135 katika siku tatu za mapumziko ya Siku ya Qingming, ambayo ni ongezeko la asilimia 6.8 kuliko mwaka uliopita, wakati huohuo matumizi ya utalii yameongezeka kwa asilimia 6.6 hadi kufikia yuan karibu bilioni 61.37 (dola za Marekani bilioni 8.9).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha