Habari picha: Mkulima mpya wa China aleta uvumbuzi na ujuzi shambani (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 13, 2026
Habari picha: Mkulima mpya wa China aleta uvumbuzi na ujuzi shambani
Luo Yu (kushoto) akitoa kielelezo wakati wa kupiga picha ya video fupi katika Eneo la Huatang, Chenzhou, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Aprili 10, 2026. (Xinhua/Xue Yuge)

Luo Yu, aliyezaliwa mwaka 1997, alihitimu na shahada ya uuguzi, lakini sasa amekuwa "mkulima mpya" mwenye uwezo ambaye anakumbatia teknolojia ya kisasa na kuingiza mawazo na ujuzi wa kivumbuzi katika kilimo.

Luo na mumewe awali walikuwa wakifanya shughuli ya nyumba ya kuwapokea wageni katika Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China miaka minne iliyopita. Wanandoa hao waliamua kufunga nyumba hiyo ya kuwapokea wageni na kurudi maskani yao katika Mkoa wa Hunan, katikati mwa China ili kupunguza mzigo wa baba yake Luo, ambaye alikuwa akishughulikia kazi ya kilimo kwenye shamba la hekta 3000 hivi.

Kuanzia mwanzo kabisa, Luo alijifunza kuendesha mashine za kilimo na kununua zana na vyombo vinavyofaa kwa ardhi ya eneo hilo. Wanandoa hao waliunganisha na kusawazisha ploti zilizokuwa zimetawanyika na kuziboresha kuwa ardhi ya hali ya juu ya kilimo. Luo pia alianzisha timu ya kutoa huduma za mzunguko mzima wa kilimo kwa wakulima wanaoishi pembezoni mwa eneo hilo.

Ukubwa wa ardhi zilizolimwa chini ya uangalizi wao ulifikia jumla ya hekta 296.15 hivi mwaka jana, ambapo walitoa nafasi za ajira kwa familia za wakulima zaidi ya 200.

Luo bado anatafuta maendeleo zaidi kwa kupitia vyombo vipya vya habari, na anapanga kuzindua chapa yake mwenyewe. "Natumai vijana wengi zaidi watakuwa na nia ya kuwa 'wakulima wapya' na kuleta mabadiliko kwa ari na hekima yao," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha