Lugha Nyingine
Habari picha: Mkulima mpya wa China aleta uvumbuzi na ujuzi shambani (5)
![]() |
| Luo Yu akipiga picha ndani ya kibanda cha kilimo cha kisasa cha kijani katika Eneo la Huatang, Chenzhou, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Aprili 9, 2026. (Xinhua/Xue Yuge) |
Luo Yu, aliyezaliwa mwaka 1997, alihitimu na shahada ya uuguzi, lakini sasa amekuwa "mkulima mpya" mwenye uwezo ambaye anakumbatia teknolojia ya kisasa na kuingiza mawazo na ujuzi wa kivumbuzi katika kilimo.
Luo na mumewe awali walikuwa wakifanya shughuli ya nyumba ya kuwapokea wageni katika Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China miaka minne iliyopita. Wanandoa hao waliamua kufunga nyumba hiyo ya kuwapokea wageni na kurudi maskani yao katika Mkoa wa Hunan, katikati mwa China ili kupunguza mzigo wa baba yake Luo, ambaye alikuwa akishughulikia kazi ya kilimo kwenye shamba la hekta 3000 hivi.
Kuanzia mwanzo kabisa, Luo alijifunza kuendesha mashine za kilimo na kununua zana na vyombo vinavyofaa kwa ardhi ya eneo hilo. Wanandoa hao waliunganisha na kusawazisha ploti zilizokuwa zimetawanyika na kuziboresha kuwa ardhi ya hali ya juu ya kilimo. Luo pia alianzisha timu ya kutoa huduma za mzunguko mzima wa kilimo kwa wakulima wanaoishi pembezoni mwa eneo hilo.
Ukubwa wa ardhi zilizolimwa chini ya uangalizi wao ulifikia jumla ya hekta 296.15 hivi mwaka jana, ambapo walitoa nafasi za ajira kwa familia za wakulima zaidi ya 200.
Luo bado anatafuta maendeleo zaidi kwa kupitia vyombo vipya vya habari, na anapanga kuzindua chapa yake mwenyewe. "Natumai vijana wengi zaidi watakuwa na nia ya kuwa 'wakulima wapya' na kuleta mabadiliko kwa ari na hekima yao," amesema.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
