Hospitali ya Mji wa Tianjin, China yatumia roboti kwenye upasuaji wenye maumivu kidogo sana (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2026
Hospitali ya Mji wa Tianjin, China yatumia roboti kwenye upasuaji wenye maumivu kidogo sana
Daktari akiendesha roboti ya upasuaji ya da Vinci katika Taasisi ya Saratani na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Tianjin mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Aprili 19, 2026. (Xinhua/Li Ran)

Katika miaka ya hivi karibuni, Taasisi ya Saratani na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Tianjin katika Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China imeendelea kusukuma mbele maendeleo katika upasuaji wenye maumivu kidogo sana. Hospitali hiyo kwa sasa ina roboti tatu za upasuaji za da Vinci na imeshafanya upasuaji zaidi ya mara 10,000 kwa kutumia mfumo huo, na kuanzisha mfumo wa taaluma mbalimbali za matibabu yenye maumivu kidogo sana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha