Kijiji cha Jinling mkoani Zhejiang China chaendeleza shughuli za utalii za kuhusisha utamaduni wa kijiji chenye mazingira mazuri ya asili (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 27, 2026
Kijiji cha Jinling mkoani Zhejiang China chaendeleza shughuli za utalii za kuhusisha utamaduni wa kijiji chenye mazingira mazuri ya asili
Picha iliyopigwa Aprili 24, 2026 ikionyesha maua ya azalea ya milimani yaliyochanua katika Kijiji cha Jinling, Wilaya ya Chun'an mkoani Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Xu Yu)

Kijiji cha Jinling, kilichopo kwenye mwinuko wa mita zaidi ya 1,000 juu ya usawa wa bahari, ni moja ya vijiji vilivyoko kwenye mwinuko wa juu zaidi katika Wilaya ya Chun'an mkoani Zhejiang, mashariki mwa China. Katika miaka ya hivi karibuni, kijiji hicho kimetumia vya kutosha maliasili zake nyingi kwa kuendeleza shughuli za utalii za kuhusisha utamaduni wa kijiji chenye mazingira mazuri ya asili.

Kwa kupitia kuboresha miundombinu, kujenga maeneo ya kupiga kambi na majukwaa ya kutazama mandhari, vilevile kuhimiza maendeleo ya nyumba za kuwapokea wageni, Kijiji hicho cha Jinling hatua kwa hatua kimeanzisha shughuli za utalii za kutembea kwa miguu, kutazama mandhari na kupumzika wakati wa majira ya joto, hali ambayo imeongeza mapato kwa wanakijiji wa eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha