Mji wa Shenzhen wajenga "mduara wa huduma za malezi ya watoto wa dakika 15" ili kupunguza mzigo wa familia (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2026
Mji wa Shenzhen wajenga
Mwalimu akicheza michezo na watoto kwenye kituo cha chekechea katika Jumuiya ya Makazi ya Meihe, Futian, Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Aprili 17, 2026. (Xinhua/Liang Xu)

Mji wa Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China unajenga "mduara wa huduma za malezi ya watoto wa dakika 15" unaohudumia siku 1,000 za kwanza za maisha ya mtoto ili kupunguza mzigo wa familia na kuhimiza uzazi zaidi.

Kwa kuungwa mkono na serikali, jamii na watoa huduma za kitaalamu pamoja, mji huo umekuwa ukifanyia kazi mageuzi ya vituo vya umma ili kuunda huduma za malezi ya watoto zinazopatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na zilizo karibu na nyumba za watoto.

Kwa sasa, Shenzhen imeanzisha nafasi 109,000 za huduma za malezi ya watoto zenye angalau kituo kimoja cha chekechea cha umma au kituo cha huduma za chekechea katika kila kitongoji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha