Mafundi wahifadhi sanaa za rangi za urithi wa utamaduni usioshikika katika Mkoa wa Shandong, China (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2026
Mafundi wahifadhi sanaa za rangi za urithi wa utamaduni usioshikika katika Mkoa wa Shandong, China
Picha hii iliyopigwa Mei 26, 2026 ikionyesha kazi ya sanaa za rangi. (Xinhua/Zhu Zheng)

Katika wakati wa mwanzo wa majira ya joto, joto kali imekuwa ikijaa katika karakana ya uzalishaji ya "Heshunlu", chapa ya sanaa za rangi ambayo imekuwa na historia ndefu katika Eneo la Boshan la Mji Zibo, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China.

Sun Yunhao na mafundi wenzake wanatumia mabomba ya chuma yenye matundu kuchukua raslimali za kioo zilizoyeyushwa kutoka kwenye tanuru inayozidi nyuzi joto 1,400. Wanapuliza, kuunda maumbo, kunyoosha na kuzungusha, na kuunda kwa haraka sanaa mbalimbali kwa kufuata hali ya kimiminika na unyumbufu ya raslimali za kioo zilizoyeyushwa.

Eneo hilo la Boshan, Sun Yunhao anakoishi, linasifiwa kuwa chimbuko la sanaa za rangi nchini China likiwa na historia ya kutengeneza sanaa za rangi kwa maelfu ya miaka. Sanaa za rangi za Boshan zilianzia katika Enzi ya Zhou Magharibi (1046 KK-771 KK), ilistawi katika kipindi cha enzi za Han (202 KK-220 BK) na Tang (618-907), na kufikia kilele chake katika enzi za Ming (1368-1644) na Qing (1644-1911).

Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, sanaa za rangi za Boshan ziliingia katika uzalishaji mkubwa. Mwaka 2008, "Ufundi wa Kutengeneza Sanaa za Rangi za Boshan Kwenye Tanuri" uliwekwa kwenye orodha ya mali ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China.

Sun Yunhao aliyezaliwa mwaka 1977 katika familia ya mafundi wa sanaa za rangi, tangu alipokuwa utotoni, alijifunza ufundi stadi wa kijadi kutoka kwa baba yake Sun Jijie, ambaye ni mbobezi wa sanaa za rangi za China. Kutoka uwiano wa malighafi hadi udhibiti wa halijoto ya moto kwenye tanuri, na kutoka usanifu wa sanaa hadi uundaji wake kwenye tanuri, uzoefu wa miaka mingi umemwezesha kuinua " sanaa ya rangi inayoundwa kwenye tanuri " hadi kiwango kipya cha juu. Kupitia juhudi zake bila kulegalega, kazi za sanaa za rangi za Sun Yunhao zimepewa tuzo kadhaa muhimu katika sekta mbalimbali.

Mwezi Machi, 2025, Sun Yunhao alitambuliwa rasmi kuwa mrithi mwakilishi wa kitaifa wa "Ufundi wa Kutengeneza Sanaa za Rangi za Boshan Kwenye Tanuri". Sun alikuwa mtangulizi wa kuanzisha darasa la mali ya sanaa za rangi za urithi wa utamaduni usioshikika kwenye msingi wa ufundi wa sanaa za kijadi, huku akiiga dhana na ufundi wa kutengeneza glasi za magharibi , na kujaribu kufanya mafungamano ya taaluma za kuvuka mpaka kati ya sanaa za rangi na madini, mbao, na kauri. Hadi sasa amewaandaa wabobezi 13 wa sanaa na ufundi wa daraja la kitaifa na wa mkoa na mafundi wakuu zaidi ya 30.

Siku hizi, kuna kampuni 13 ya uzalishaji wa sanaa za rangi na studio 65 husika za sanaa katika eneo hilo la Boshan. Zaidi ya asilimia 70 ya bidhaa zao zinasafirishwa kwenda nchi za Ulaya, Marekani, n.k.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha