Viongozi wa E3 waunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja ya Ukraine-Russia na kutaka kusimamisha mapigano (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2026
Viongozi wa E3 waunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja ya Ukraine-Russia na kutaka kusimamisha mapigano
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (wa pili kulia), Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (wa kwanza kulia), Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz (wa kwanza kushoto) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakizungumza katika Mtaa No.10 wa Downing baada ya mkutano wao jijini London, Uingereza, Juni 7, 2026. (Picha na Stephen Chung/Xinhua)

LONDON - Viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, kwa pamoja wakijulikana kwa jina la E3, wameeleza kuunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Ukraine na Russia yenye lengo la kufikia kusimamisha mapigano na kusukuma mbele mazungumzo ya amani, kufuatia mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky jijini London.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz wametoa taarifa ya pamoja na Zelensky baada ya mkutano wao huo wa siku ya Jumapili, wakisema wanaunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Ukraine an Russia pamoja na ushiriki wa kivitendo wa Marekani na Ulaya.

Viongozi hao wanne wametoa wito wa kusimamisha mapigano mara moja na kikamilifu, wakisema mstari wa sasa wa mbele unapaswa kutumika kama mwanzo wa mazungumzo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ulaya inapaswa kuchukua jukumu muhimu katika mchakato huo wa amani, huku juhudi husika zikifanywa kwa uratibu wa karibu na Ukraine, washirika wa Ulaya na Marekani.

Viongozi hao pia wamejadili mipango ya usalama kwa ajili ya Ukraine baada ya kusimamishwa kwa mapigano. Taarifa hiyo imesema maslahi ya kiusalama ya Ulaya yanapaswa kulindwa katika makubaliano yoyote na imebainisha kuwa masuala yanayohusiana na Umoja wa Ulaya na NATO yatahitaji idhini ya nchi wanachama wao husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha