Lugha Nyingine
Mjasiriamali kijana wa China ajitolea kwa ustawi wa kijiji kupitia kufanya kazi kwa bidii (2)
![]() |
| Picha iliyopigwa Juni 5, 2026 ikimuonyesha Qiu Guimin akifanya kazi shambani katika Kijiji cha Nanwan cha Wilaya ya Pingnan, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China. (Xinhua/Lin Shanchuan) |
Mwaka 2016, baada ya kuhitimu kutoka chuoni, mjasiriamali kijana wa China Qiu Guimin alirudi kwenye maskani yake ya kijiji cha Wilaya ya Pingnan, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China na kuanzisha ushirika wa kilimo.
Mwaka 2020, alianza kukodi mashamba yaliyoachwa kulima kutoka kwa wanakijiji wa Kijiji cha Nanwan kwa ajili ya kilimo cha nafaka. Katika wakati wa kurejesha hali ya vilima vilivyotelekezwa na kuvifanya kuwa mashamba ya kilimo, Qiu pia alishirikiana na Kijiji cha Nanwan kufanya shughuli za kitamaduni na utalii kama vile tamasha la muziki na sherehe za Siku ya Utamaduni wa Kilimo.
Shughuli hizo zimewavutia vijana wengi kutoka nje ya kijiji hicho kufungua nyumba za kuwapokea wageni na mikahawa katika kijiji hicho, na kuingiza nguvu hai mpya katika jamii ya wakazi wa kijiji hicho.
"Kijiji kinapata matumaini kwa kuongezeka umaarufu," Qiu amesema.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
