Lugha Nyingine
China yatoa waraka juu ya usimamizi wa dunia (3)
![]() |
| Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China (SCIO) ikifanya mkutano na waandishi wa habari kuwasilisha waraka mwenye kichwa "Usimamizi wa Dunia wenye Haki na Usawa Zaidi: Kanuni, Mapendekezo na Vitendo vya China" mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 17, 2026. (Xinhua/Li Xin) |
BEIJING - Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China jana Jumatano imetoa waraka mweupe mwenye kichwa cha "Usimamizi wa Dunia wenye Haki na Usawa Zaidi: Kanuni, Mapendekezo na Vitendo vya China."
Waraka huo umechapishwa ili kutambulisha kanuni, mapendekezo na vitendo vya China juu ya usimamizi wa dunia, kujenga maafikiano mapana zaidi ndani ya jumuiya ya kimataifa, kuhakikisha kukabiliana kwa ubora zaidi na changamoto za kimataifa, na kujenga mfumo wa usimamizi wa dunia wenye haki na usawa zaidi.
Katika zama mpya, Rais Xi Jinping alitoa maono ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu. Katika kuhimiza mfumo wa utawala wa kimataifa wenye sifa ya mashauriano mapana na mchango wa pamoja kwa manufaa ya pamoja, ametoa wito wa ushirikiano wa kweli wa pande nyingi ili kujenga dunia ya pande nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote, kwa mujibu wa waraka huo.
Unasema kwamba mwaka 2025, Xi alitoa Pendekezo la Usimamizi wa Dunia (GGI), ambalo limeandaliwa ili kutoa suluhisho la China kwa maswali mawili muhimu ya zama hii: ni aina gani ya mfumo wa usimamizi wa dunia unapaswa kuanzishwa, na ni kwa namna gani usimamizi wa dunia unaweza kufanyiwa mageuzi na kuboreshwa.
Baada ya kuanzishwa kwake, GGI ilipata uungwaji mkono haraka kutoka nchi na mashirika ya kimataifa karibu 160, huku nchi zaidi ya 60 zikijiunga na Kundi la Marafiki wa Usimaizi wa Dunia. Jumuiya ya kimataifa inaamini kwamba GGI inatuma ishara dhahiri: kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kuunganisha nguvu, na kufuata mustakabali wa haki, waraka huo unasema.
Kwa mujibu wa waraka huo, GGI inaendana na mwelekeo unaozidi kuongezeka wa kuelekea demokrasia kubwa zaidi katika uhusiano ya kimataifa na inaimarisha imani ya kimataifa katika kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi. Inatoa dira dhahiri na inayoweza kufikiwa ya kuboresha usimamizi wa dunia, kuleta utulivu muhimu na nishati chanya kwa dunia yenye misukosuko.
Waraka huo unasema China imependekeza GGI ili kuharakisha ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa dunia wenye haki na usawa zaidi. Unasema kudumisha kithabiti mamlaka na hadhi ya Umoja wa Mataifa ni muhimu kwa utekelezaji mzuri wa pendekezo hilo.
Mbali na utangulizi na hitimisho, waraka huo una sehemu tano: "Dunia ya Leo Inakabiliwa na Changamoto Kali na Ngumu," "Pendekezo la Usimamizi wa Dunia Linakabiliana na Changamoto za Nyakati Zetu," "Mchango wa China katika Kuhimiza Utawala wa Kimataifa," "Kuongoza Mwelekeo wa Mabadiliko Kuelekea Mustakabali Mzuri," na "Kusonga Mbele Bega kwa Bega katika Wakati Muhimu katika Historia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




