Hafla ya kumwabudu Fuxi yafanyika Tianshui katika Mkoa wa Gansu, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 22, 2026
Hafla ya kumwabudu Fuxi yafanyika Tianshui katika Mkoa wa Gansu, China
Picha iliyopigwa Juni 21, 2026 ikionyesha hafla ya kumwabudu Fuxi, babu wa kwenye simulizi za kale wa taifa la China, katika Mji wa Tianshui, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China. (Picha na Liu Keying/Xinhua)

Hafla ya kumwabudu Fuxi, babu wa kwenye simulizi za kale wa taifa la China, ambaye anaabudiwa kwa mchango wake wa kufundisha watu kuhusu uvuvi, uwindaji na ufugaji, imefanyika jana Jumapili katika Mji wa Tianshui, unaochukuliwa kuwa ni mahali pa kuzaliwa kwa babu huyo, mkoani Gansu, kaskazini magharibi mwa China.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za kihistoria, shughuli ya kila mwaka ya kumwabudu Fuxi imekuwa na historia ya miaka zaidi ya 2,000. Shughuli hiyo iliorodheshwa kuwa mali ya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China mwaka 2006.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha