Makamu Rais wa China akutana na mwenzake wa Afrika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2026

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile mjini Beijing, China, Juni 23, 2026. (Xinhua/Li Tao)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile mjini Beijing, China, Juni 23, 2026. (Xinhua/Li Tao)

BEIJING - Makamu Rais wa China Han Zheng amekutana na Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile Jumanne mjini Beijing.

Han amekumbuka yeye pamoja na Mashatile waliongoza mkutano wa tisa wa wajumbe wote wa Kamisheni ya Pande Mbili za China na Afrika Kusini mwezi Machi, na amesema mkutano huo ulipata mafanikio mazuri.

Han amesema, "Pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza zaidi maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa na marais wa nchi zetu, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, na kuhimiza utekelezaji zaidi wa matokeo ya mkutano huo."

Amesema China na Afrika Kusini zikiwa nchi wanachama wa BRICS na G20, zinapaswa kuimarisha uratibu wa kimataifa na kwa pamoja kufanya kazi za kuhimiza hamasa katika kuboresha usimamizi wa uchumi duniani.

Kwa upande wake Mashatile amesema Afrika Kusini siku zote inafanya juhudi zaidi katika kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na kuongeza ushirikiano wa kunufaishana na China.

Amesema Afrika Kusini inafuata sera ya kuwepo kwa China moja na inapenda kufanya juhudi pamoja na China ili kuungana mkono katika kulinda maslahi yao makubwa.

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile mjini Beijing, China, Juni 23, 2026. (Xinhua/Li Tao)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile mjini Beijing, China, Juni 23, 2026. (Xinhua/Li Tao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha