Mashine za teknolojia mahiri za China zaduwaza watembeleaji kwenye maonyesho nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2026

Muuzaji wa China (kushoto) akimsaidia mtembeleaji kuendesha forklift iliyotengenezwa China kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi ya Afrika 2026 jijini Nairobi, Kenya, Juni 19, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

Muuzaji wa China (kushoto) akimsaidia mtembeleaji kuendesha forklift iliyotengenezwa China kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi ya Afrika 2026 jijini Nairobi, Kenya, Juni 19, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

NAIROBI - Peter Wairegi alisimama pembeni ya ekskaveta iliyotengenezwa na Zoomlion, kampuni ongozi ya mashine za ujenzi ya China, akichunguza kwa makini mfumo wake wa udhibiti wa AI na muundo mzuri kwenye maonyesho ya mashine jijini Nairobi, Kenya.

Wairegi, mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya ya Mawakala Wataalamu wa Uuzaji Majengo ya Kenya, ni miongoni mwa mamia ya watembeleaji na wanunuzi waliohudhuria Maonyesho ya hivi karibuni ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi, Mashine za Uchimbaji Madini, Kilimo na Vipuri vya Magari, Bidhaa za Kielektroniki na bidhaa za vifaa vya chuma za Afrika.

"Nimefurahi kutembelea maonyesho haya na naweza kuona kampuni nyingi za China ambazo zimeleta vifaa na uvumbuzi mpya kwa mfumo mzima wa mali isiyo hamishika, hasa katika majengo na ujenzi," amesema Wairegi.

"Katika maonyesho haya, nimevutiwa kuona mashine za kuinua nyenzo kwenye majengo marefu, lifti, jenereta, ekskaveta za ujenzi wa barabara, na magreda," ameongeza.

Wairegi amesema atahamasisha wadau katika sekta ya mali isiyohamishika, kama vile waendelezaji miradi, kutembelea maonyesho hayo na kufahamu kuhusu mashine na vifaa vya kisasa vilivyotengenezwa China ambavyo vimeletwa nchini Kenya na katika soko pana la Afrika.

Mtembeleaji (katikati) akimuuliza mwonyeshaji bidhaa kuhusu pikipiki iliyotengenezwa China kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi ya Afrika 2026 jijini Nairobi, Kenya, Juni 19, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

Mtembeleaji (katikati) akimuuliza mwonyeshaji bidhaa kuhusu pikipiki iliyotengenezwa China kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi ya Afrika 2026 jijini Nairobi, Kenya, Juni 19, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

“Wengi wa wajumbe wa jumuiya wanapendelea bidhaa za China kama vile vigae, madirisha na makabati wanapojenga nyumba”, amesema, akiongeza kuwa anatarajia kujenga uhusiano imara zaidi na watengenezaji vifaa vya ujenzi wa China.

Kampuni zaidi ya 200 za China zinazoshughulika na mashine nzito, vipuri vya magari, pikipiki za umeme, suluhu za nishati safi na teknolojia za kutibu maji machafu zinaonyesha bidhaa zao kwenye maonyesho hayo.

Anthony Njagi, meneja mauzo na uendeshaji katika Kampuni ya Vifaa ya CAMCO ya Kenya, msambazaji wa Kenya wa mashine za kilimo, vifaa, na jenereta kutoka China, amesema watembeleaji wengi wamevutiwa na matrekta yaliyoonyeshwa kwa muundo wao maridhawa na sifa za kipekee.

"Uwepo wa mashine za kilimo za China barani Afrika ni wenye kuleta mabadiliko makubwa kwa sababu ni nafuu, zinadumu kwa muda mrefu na zimetengenezwa mahsusi kwa soko la Afrika," amesema Njagi.

Amesema maonyesho hayo yanatoa fursa ya kuonyesha umaarufu wa vifaa vya kilimo vya China miongoni mwa wakulima, wakusanyaji na wasindikaji wa mazao ya kilimo wenyeji.

Wafanyakazi wa kampuni ya pikipiki za umeme wakipiga picha kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi ya Afrika 2026 jijini Nairobi, Kenya, Juni 19, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

Wafanyakazi wa kampuni ya pikipiki za umeme wakipiga picha kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Mashine za Ujenzi ya Afrika 2026 jijini Nairobi, Kenya, Juni 19, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

Maonyesho hayo yanayofanyika chini ya kaulimbiu ya "Uzalishaji Mahiri Afrika, Mustakabali wa Pamoja," yamepongezwa na maafisa wa Kenya kwa kupata mafanikio mapya katika ushirikiano wa biashara na viwanda na China.

Juma Mukhwana, katibu mkuu katika Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda ya Kenya, amesema Kenya ina nia ya kutumia ipasavyo vifaa vya kisasa kutoka China ili kuboresha sekta muhimu kama vile kilimo, miundombinu na ujenzi.

Kwa mujibu wa Mukhwana, serikali imeanzisha motisha za kifedha na kiusimamizi ili kuvutia mitaji, teknolojia na vifaa vya kisasa kutoka China ili kuhimiza utengenezaji bidhaa wa kijani, kuongeza thamani kwa mazao ya kilimo na vyombo vya usafiri vyenye kutumia kaboni chache.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha