Lugha Nyingine
Xi Jinping atoa wito wa kuchukua hatua halisi zaidi za kuhimiza mambo ya kisasa ya Kilimo na Vijiji

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akifahamishwa kuhusu mavuno ya ngano, upandaji wa mahindi, na pembejeo za kilimo katika Kijiji cha Dongyujia cha Eneo la Lingcheng la Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
DEZHOU - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), kwenye ziara yake ya ukaguzi Jumatano katika Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China ametoa wito wa kuchukua hatua halisi zaidi za kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya kisasa ya kilimo na vijiji.
Xi amesema ni lazima kufanya juhudi za kuongeza uwezo wa jumla wa uzalishaji, ubora wa mazao, na ufanisi wa kilimo, kuhakikisha utoaji wa nafaka na mazao muhimu ya kilimo, kujenga vijiji kuwa vya kupendeza na vyenye hali ya maafikiano kwa kufuata hali halisi ya maeneo husika, na kuwawezesha wakulima kujenga maisha mazuri zaidi kwa kupitia kufanya kazi kwa bidii na hekima.
Katika Kijiji cha Dongyujia, Xi alifahamishwa kuhusu mavuno ya ngano, upandaji wa mahindi, na pembejeo za kilimo za huko. Pia alitembelea kuingia shambani na kufanya mazungumzo ya kikunjufu na wakulima wa nafaka, waendesha mashine za kilimo na mafundi wa kilimo.
Xi amesisitiza kwamba kuhakikisha utoaji tulivu wa nafaka na mazao mengine ya kilimo ni jukumu kuu katika uzalishaji wa kilimo, na amesisitiza juhudi za kutekeleza sera zote za uungaji mkono kwa uzalishaji wa nafaka ili kupata mavuno ya nafaka ya mwaka mzima.
Xi pia ametoa wito wa juhudi za kuboresha miundombinu ya kilimo na kuimarisha uwezo wa kuzuia, kupunguza na kuokoa maafa katika kilimo.
Baadaye, Xi alitembelea Kijiji cha karibu cha Xiyujia, ambapo aliuliza kwa undani kuhusu hali ya oganaizesheni za Chama za kijiji hicho na hali ya utoaji wa huduma za umma. Pia alitembelea maonyesho ya mazao ya kilimo na bidhaa zile zinazotokana nayo huko.
Xi alielezea matumaini kwamba oganaizesheni za Chama za kijiji zitafanya kazi zaidi za kuongoza ujenzi wa Chama na kupata mafanikio mapya katika kujenga kijiji cha kupendeza na chenye hali ya maafikiano, na ya kufaa kuishi na kuzalisha mali.
Ndani ya nyumba ya mwanakijiji Yu Xinhui, Xi aliketi na familia yake, na kuuliza kuhusu maisha yao ya kila siku, hali ya kazi, mapato, afya ya wazee, na elimu ya watoto wao.
Rais Xi amesema kwamba wanachama wa Chama na makada lazima wafanye juhudi zaidi za kuleta manufaa kwa watu, kuleta matokeo halisi kwa ustawi wa watu, na kuwasaidia kushinda taabu, ili kuwawezesha watu kuongeza hisia zao za kupata na kuridhika, kuona furaha na usalama.

Rais wa China Xi Jinping, akifahamishwa kuhusu miundombinu ya kilimo katika Kijiji cha Dongyujia cha Eneo la Lingcheng la Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping, akiwa ameingia shambani na kufanya mazungumzo ya kikunjufu na wakulima wa nafaka, waendesha mashine za kilimo na mafundi wa kilimo katika Kijiji cha Dongyujia cha Eneo la Lingcheng la Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping, akiwa ameketi na familia ya mwanakijiji Yu Xinhui kuuliza kuhusu hali ya maisha yao ya kila siku nyumbani kwao katika Kijiji cha Xiyujia cha Eneo la Lingcheng la Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping, akizungumza na wanakijiji alipofanya ziara katika Kijiji cha Xiyujia cha Eneo la Lingcheng la Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping, akizungumza na wanakijiji alipofanya ziara katika Kijiji cha Xiyujia cha Eneo la Lingcheng la Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



