Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China ahutubia mkutano wa wajumbe wote wa kufunguliwa kwa Jukwaa la Davos

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia mkutano wa wajumbe wote wa kufunguliwa kwa Mkutano wa 17 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya, ambao pia unajulikana kuwa ni Jukwaa la Davos la Majira ya Joto, uliofanyika Dalian, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, Juni 24, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
DALIAN - Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametoa hotuba maalum kwenye mkutano wa wajumbe wote wa kufunguliwa kwa Mkutano wa 17 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya, ambao pia unajulikana kuwa ni Jukwaa la Davos la Majira ya Joto, katika mji wa pwani wa Dalian kaskazini mashariki mwa China jana Jumatano.
Mada kuu ya mkutano huo ni "Uvumbuzi wa Kiwango," mkutano huo umefanyika kuanzia tarehe 23, Juni na utamalizika leo tarehe 25, Juni, washiriki zaidi ya 1,700 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 90 wamekusanyika kwenye jukwaa hilo, washiriki ambao wanajadili mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na maendeleo ya uchumi wa China katika kipindi kijacho pamoja na namna ya kubadili maendeleo ya teknolojia kuwa maslahi halisi ya kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



