Lugha Nyingine
Tetemeko la ardhi lenye nguvu kubwa latokea mara mbili Venezuela, vifo vyafikia 235, majeruhi 4,300
Picha hii iliyopigwa Juni 25, 2026 ikionyesha majengo yaliyoharibiwa katika Jimbo la La Guaira, Venezuela. (Picha na Marcos Salgado/Xinhua)
CARACAS - Tetemeko kubwa la ardhi limetokea kwa mara mbili mfululizo nchini Venezuela jana Alhamisi (Jumatano kwa saa za Amerika) na kuufanya mji mkuu Caracas kukumbwa mara mbili na tetemeko la ardhi lenye nguvu kubwa, na kusababisha vifo vya watu 235, wengine 4300 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Venezuela.
Akizungumza kupitia televisheni ya serikali ya Venezuela, Mwenyekiti wa Bunge la Taifa la nchi hiyo Jorge Rodriguez amesema, nchi hiyo inashindana na wakati kwa kuokoa watu waliojeruhiwa na waliokumbwa na janga.
“Venezuela ilikuwa imerekodi matetemeko ya ardhi yaliyotokea kwa mara 138 ya baada ya tetemeko kubwa hadi kufikia Alhamisi alasiri,” amesema Rodriguez, na kuongeza kuwa kwa sababu ya kuendelea kwa matetemeko ya baada ya tetemeko kubwa la ardhi, serikali ya Venezuela imeyatangaza maeneo kadhaa, likiwemo Jimbo la La Guaira, kuwa maeneo ya maafa.
Amesema majengo yasiyopungua 346 yamebomolewa, ikiwa ni pamoja na hospitali nane, ambazo baadhi yake watu wamelazimika kuhamishwa.
Waandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua wameripoti kutikisika kwa madirisha na kuangushwa kwa rafu za vitabu ndani ya nyumba za wakazi katika mji mkuu wa nchi hiyo, na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha nyumba zilibomoka katika mitaa ya Caracas.
Vyombo vya habari vya Colombia pia vimeripoti kwamba tetemeko la adhiri lilihisiwa sana katika miji kadhaa katika nchi hiyo ya jirani ya Venezuala.
Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani (USGS) imeripoti tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 lilitokea saa 22:04 GMT Jumatano, dakika moja tu baadaye likifuatiwa na tetemeko lingine la ardhi lenye nguvu zaidi la ukubwa wa 7.5. Yote mawili yametokea karibu na mji wa pwani wa Moron, umbali wa kilomita takribani 160 magharibi mwa Caracas.
Watu wakiwatafuta manusura chini ya vifusi katika Jimbo la La Guaira, Venezuela, Juni 25, 2026. (Picha na Marcos Salgado/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



