Afghanistan yasema mashambulizi ya Pakistan ya kupiga mabomu kutoka angani yasababisha vifo vya watu 36 katika majimbo ya mpakani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2026

Watu wakiangalia jengo lililobomolewa baada ya shambulio la kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya Jimbo la Paktia, Afghanistan, Juni 29, 2026. (Picha na Yusuf Mangal/Xinhua)

KABUL/ISLAMABAD - Maofisa wa serikali ya Afghanistan wamesema kwamba mashambulizi ya Pakistan ya kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya mashariki mwa Afghanistan yamasababisha vifo vya watu wasiopungua 36 na wengine 163 kujeruhiwa.

Hamdullah Fitrat, naibu msemaji wa serikali ya Afghanistan, ameandika kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa X Jumatatu kwamba mashambulizi hayo yalitokea Jumapili usiku dhidi ya majimbo ya Paktia, Paktika na Kunar, ambayo yote yanapakana na Pakistan.

Mapema, msemaji wa serikali ya Afghanistan Zabihullah Mujahid alilaani vikali mashambulizi hayo.

Waziri wa Habari na Utangazaji wa Serikali Kuu ya Pakistan Attaullah Tarar alisema mapema kwamba Pakistan ilianzisha operesheni ya ardhini na kufanya mashambulizi ya kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya magaidi wa kundi la Tehreek-e-Taliban Pakistan lililopigwa marufuku na kundi lililojitenga nalo la Jamaat-ul-Ahrar kwenye maeneo ya mpaka wa Pakistan na Afghanistan.

“Magaidi ishirini na tisa wameuawa na walihusika katika matukio kadhaa ya kigaidi ya hivi karibuni dhidi ya raia wasio na hatia na vyombo vya utekelezaji wa sheria vya Pakistan,” waziri huyo wa Pakistani amesema.

Picha hii ikionesha jengo lililobomolewa baada ya shambulio la kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya Jimbo la Paktia, Afghanistan, Juni 29, 2026. (Picha na Yusuf Mangal/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha