Xi apongeza miaka 105 ya “mafanikio makubwa” ya CPC, ahimiza kuijenga China ya mambo ya kisasa ya kijamaa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 02, 2026
Xi apongeza miaka 105 ya “mafanikio makubwa” ya CPC, ahimiza kuijenga China ya mambo ya kisasa ya kijamaa
Rais wa China Xi Jinping, akiwatunuku Nishani ya Julai Mosi, ambayo ni heshima ya juu zaidi ya Chama kwa wanachama wa mfano wa kuigwa wa CPC, Beijing, China, Julai 1, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amepongeza historia ya miaka 105 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kuielezea kuwa ni "mafanikio makubwa ya kustaajabisha zaidi" ya taifa la China na amekihimiza Chama kuhimiza kazi ya utekelezaji wa mpango wa kuijenga China kuwa nchi ya mambo ya kisasa ya kijamaa.

Akihutubia mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa CPC mjini Beijing jana Jumatano, Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito wa kuwataka wanachama wa Chama kuwa na imani thabiti na kufanya juhudi bila kulegalega, na kutimiza majukumu ya Chama katika zama mpya na katika safari mpya.

Chama cha CPC kilianzishwa mwaka 1921, wakati ambapo China ilikuwa nchi dhaifu iliyokuwa imekumbwa na udhalilishaji wa nchi za nje na umaskini. Chama hicho kimekua kutoka kundi dogo la wanachama zaidi ya 50 hadi sasa kuwa chama kikubwa zaidi chenye ushawishi mkubwa duniani .

Xi amesisitiza umuhimu wa kutimiza lengo la kuijenga China kuwa nchi ya mambo ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote ifikapo katikati ya karne hii.

"Muda haumsubiri mtu yeyote, na wala historia haifanyi hivyo," amesema.

Pia ametoa wito kwa Chama kizima kukabiliana kwa bidii na hatari na changamoto kwenye njia ya kusonga mbele.

Ameonya kuwa, "Maendeleo ya China sasa yako katika kipindi ambacho fursa za kimkakati zipo kwa pamoja na hatari na changamoto, ambapo hali zisizo na uhakika na zisizoweza kutabirika zinazidi kuongezeka. Lazima tuko tayari kuhimili kila wakati majaribu makubwa ya upepo mkali na mawimbi yenye misukosuko, na hata dhoruba kali."

Amesema kadiri mabadiliko makubwa ambayo hayajaonekana katika miaka 100 iliyopita yanavyozidi kutokea kwa kasi, dunia imeingia katika kipindi kipya cha msukosuko na mabadiliko, huku binadamu wakisimama tena kwenye njia panda za chaguo la kihistoria.

Kwa mujibu wa takwimu mpya, Chama cha CPC sasa kimekuwa na wanachama karibu milioni 101.29 na oganaizesheni za Chama za mashinani zimefikia milioni 5.43.

Katika mkutano huo, Xi alitunuku Nishani ya Julai Mosi, ambayo ni heshima ya juu zaidi ya Chama, ambapo watu wanane walipokea heshima hiyo mwaka huu, ikiwa ni pamoja na msuluhishaji mashinani, askari mstaafu, kada wa Chama wa kijiji, daktari wa kijijini, mfanyakazi wa eneo la wakazi , mtaalamu wa kilimo, mtaalamu wa uhandisi wa mashine, na mtaalamu wa uhandisi wa kusafisha mafuta ambaye ametunukiwa heshima hiyo baada ya kifo chake.

Wanachama, wafanyakazi wa kazi za Chama, na oganaizesheni bora za Chama za mashinani kutoka sehemu mbalimbali nchini China pia wamesifiwa kwenye mkutano huo wa watu 3,000.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha