Manowari za Jeshi la Ukombozi wa umma la China (PLA) zaanza ziara ya kwanza Hong Kong (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2026
Manowari za Jeshi la Ukombozi wa umma la China (PLA) zaanza ziara ya kwanza Hong Kong
Manowari yenye makombora ya kuongozwa, Nanning, ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ikielekea kwenye kambi ya kikosi cha majini cha PLA kilichoko Hong Kong katika Kisiwa cha Stonecutters, huko Hong Kong, kusini mwa China, Julai 2, 2026. (Xinhua/Zhu Wei)

HONG KONG – Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) umesherehekea maadhimisho ya miaka 29 tangu kurudi China kwa ziara muhimu za kikosi cha manowari cha Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) jana Alhamisi.

Kikosi hicho kinajumuisha manowari zenye makombora ya kuongozwa, Nanning na Hengyang, pamoja na helikopta za kuruka na kutua kwenye manowari baharini na askari wa majini. Kikosi hicho kimeingia Hong Kong jana Alhamisi asubuhi kwa ziara ya siku tano, inayohusisha shughuli ya kufunguliwa kwa umma na shughuli za mawasiliano ya kitamaduni.

Serikali ya HKSAR ilifanya hafla ya kukaribisha kikosi hicho kwenye kambi ya kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China kilichoko Hong Kong katika Kisiwa cha Stonecutters.

Kikosi hicho cha manowari kilipita saa moja asubuhi kwenye Bandari ya Victoria katika mpangilio wa safu, kikisindikizwa na Kikosi cha Manowari cha Serikali ya mkoa wa Hong Kong na Kikosi cha Manowari cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China kilichoko Hong Kong, kabla ya kutia nanga saa 4 asubuhi. Maofisa waandamizi wa Kikosi cha Majini cha PLA na kikosi hicho cha manowari, pamoja na wajumbe wa wafanyakazi wake, walishuka na kupata mapokezi mazuri yaliyofanywa na maofisa kutoka ofisi za Serikali Kuu ya China katika HKSAR, wajumbe wa Kikosi cha PLA kilichoko Hong Kong, wakazi na wanafunzi vijana wa Hong Kong.

Hafla ya ufunguzi ilianza kwa muziki wa wimbo wa taifa, baada ya hapo Ofisa Mtendaji Mkuu wa mkoa wa Hong Kong Bw. John Lee alitoa hotuba ya makaribisho. Maofisa na wajumbe hao kisha walipanda manowari za kikosi cha majini kwa kutembelea.

Hii ni mara ya kwanza kwa manowari hizo za Nanning na Hengyang kufanya ziara mkoani Hong Kong. Manowari hizo mbili zitafunguliwa kwa wakazi wa Hong Kong na wanafunzi wa Macao kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, na kuwawezesha kupata ufahamu wa moja kwa moja kuhusu maendeleo ya ulinzi wa taifa na mambo ya kisasa ya jeshi la China katika zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha