Mkutano wa Uchumi wa Kidijitali Duniani 2026 waanza mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2026
Mkutano wa Uchumi wa Kidijitali Duniani 2026 waanza mjini Beijing
Mwonyeshaji bidhaa akionyesha mbwa roboti kwenye Maonyesho ya Sekta ya Uchumi wa Kidijitali 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China, Beijing, Julai 2, 2026. (Xinhua/Zhang Chenlin)

BEIJING - Mkutano wa Uchumi wa Kidijitali Duniani 2026 umeanza mjini Beijing jana Alhamisi, ukivutia watendaji wa kampuni, wawakilishi wa baraza la biashara, na wasomi kutoka ndani na nje ya nchi, vilevile maofisa wa ngazi ya mawaziri kutoka Kazakhstan, Colombia na Chad.

Kwenye hafla ya kufungua mkutano huo, Muungano wa Miji ya Uchumi wa Kidijitali Duniani ulitoa Ripoti ya Miji ya Uchumi wa Kidijitali Duniani 2026, ambayo inaangazia namna teknolojia za kidijitali na miji vinavyoathiriana na kusisitiza kwamba teknolojia ya kidijitali lazima iwe dhahiri kwa wakazi, ifae kwa matumizi ya biashara na iweze kupatikana kwa jamii.

Pia Kitabu cha Mifano ya Taa ya Mwongozo cha Uchumi wa Kidijitali Duniani 2026, ambacho ni chapisho la pamoja la Umoja wa Mawasiliano wa Kimataifa, Kituo cha Biashara cha Kimataifa na Muungano wa Miji ya Uchumi wa Kidijitali Duniani kimezinduliwa.

Kitabu hicho kina "mifano 13 ya mwongozo" kutoka miji ikiwemo Beijing, Jakarta, Madrid na Istanbul, kikijumuisha maeneo sita: usimamizi shirikishi wa miji ya kidijitali, huduma jumuishi za umma za kidijitali, miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi, uboreshaji wa maisha unaowezeshwa kidijitali, vyombo vya usafiri vya teknolojia za kisasa vyenye kutoa kaboni chache na ujumuishaji wa kidijitali kwa makundi yaliyo katika mazingira dhaifu.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika hadi Jumapili, pia utaandaa mfululizo wa vipindi maalum vya mada vinavyohusu AI, uendelezaji wa vipaji vya kidijitali na kuingiza mambo ya kidijitali viwandani.

Kamati ya maandalizi imesema, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, mkutano huo umeshavutia kampuni zaidi ya 10,000 na washiriki 150,000 kutoka nchi zaidi ya 200 na mashirika ya kimataifa, huku matokeo 500 yakiwa yamechapishwa hadi sasa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha