Lugha Nyingine
Hafla ya siku mbili ya kumuaga kiongozi mkuu wa zamani wa Iran yafanyika Tehran (4)
![]() |
| Jamaa akihudhuria hafla ya kumuaga Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei mjini Tehran, Iran, Julai 4, 2026. (Xinhua/Shadati) |
TEHRAN – Hafla ya kumuaga Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran Ali Khamenei imefanyika kwa siku mbili mjini Tehran, mji mkuu wa Iran kwenye ukumbi wa dua wa Imam Khomeini Mosalla kuanzia Jumamosi asubuhi, ikivutia umati mkubwa kutoka kote nchini humo.
Mwili wa kiongozi huyo marehemu na ile ya wanafamilia wake wanne, waliouawa pamoja naye katika shambulizi la Marekani na Israeli mwishoni mwa Februari, iliwekwa kwenye jukwaa lililoinuliwa.
Waombolezaji kutoka nyanja mbalimbali wamekuwa wakishikilia picha za kiongozi huyo marehemu na bendera za Iran, na kutamka kaulimbiu dhidi ya Marekani na Israeli.
Mamlaka za Iran zimeweka vizuizi vikali vya trafiki mjini Tehran, hasa karibu na Mosalla, wakati huohuo zimepanga huduma kubwa za usaidizi ili kuhudumia waombolezaji.
Shughuli hiyo ya siku mbili imekuja baada ya hafla iliyofanyika Tehran siku ya Ijumaa, ambapo maafisa wa ngazi za juu wa ndani na nje ya Iran walitoa heshima zao kwa kiongozi huyo marehemu.
Shughuli hiyo itafuatiwa na mkusanyiko wa matembezi ya mazishi leo Jumatatu mjini Tehran, ambao unatarajiwa kuvutia umati mkubwa kutoka Iran na nchi zingine za kikanda.
Kesho Jumanne, kutakuwa na hafla katika mji wa katikati mwa Iran wa Qom, na Jumatano, mwili wa kiongozi huyo utahamishiwa Iraq kwa ajili ya ibada zaidi katika miji ya Najaf na Karbala ya Iraq.
Atazikwa katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran siku ya Alhamisi wiki hii, ambayo serikali imeitangaza kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa.
Mtoto wa Ali Khamenei, Mojtaba Khamenei, alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Iran mwezi Machi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




