China na Russia kufanya mazoezi ya pamoja ya vikosi vya majini na doria ya baharini (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 06, 2026
China na Russia kufanya mazoezi ya pamoja ya vikosi vya majini na doria ya baharini
Picha hii iliyopigwa Julai 5, 2026 ikionyesha manowari ya makombora ya Varyag ya Russia itakayoshiriki kwenye mazoezi ya vikosi vya majini ya "Joint Sea-2026" ikitia nanga katika bandari ya kijeshi, huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Picha na Fengxiang/Xinhua)

BEIJING – Wizara ya ulinzi wa taifa ya China imetangaza jumapili iliyopita ikisema, vikosi vya majini vya majeshi ya China na Russia vitafanya mazoezi ya pamoja ya "Joint Sea-2026" mwezi huu kwenye maji na anga katika maeneo karibu na mji wa bandari Qingdao wa China katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China.

Wizara hiyo imesema baada ya mazoezi hayo, baadhi ya vikosi kutoka pande zote mbili vitafanya pamoja doria ya baharini katika maeneo husika ya Bahari ya Pasifiki.

Vyanzo vya habari jeshini vimesema kuwa, hadi kufikia Jumapili, manowari kutoka upande wa Russia zinazoshiriki katika mazoezi hayo zimeshawasili kwenye bandari ya kijeshi cha Qingdao, huku mkusanyiko wa vikosi vyote vinavyoshiriki ukiwa umekamilika.

Russia imetuma manowari ya makombora ya kuongozwa ya masafa marefu, manowari ya frigeti, nyambizi na meli ya uokoaji kwa ajili ya mazoezi hayo, na vikosi vya majini vya eneo la kivita la kaskakzini la China vitashiriki kwenye mazoezi hayo, vikiwa pamoja na manowari za makombora ya kuharibu yanayoongozwa, manowari ya frigeti ya makombora yanayoongozwa, manowari ya kutoa ugavi wa jumla, manowari ya uokoaji na nyambizi. Pande zote mbili pia zitatuma helikopta za kuruka na kutua kwenye manowari za majini na vikosi vya kupigana vita kwenye nchi kavu.

Kwa kuweka mkazo katika kukabiliana kwa pamoja na matishio dhidi ya usalama wa baharini, mazoezi hayo yatafanyika katika vipindi vitatu -- mkusanyiko wa vikosi, mipango bandarini na mazoezi baharini. Pande hizo mbili zitafanya upelelezi wa pamoja, ulinzi wa anga na makombora, na mazoezi ya mashambulizi ya baharini na mengineyo.

Askari kutoka pande hizo mbili pia watabadilishana mawazo kuhusu taaluma na kupanga kutembelea kwenye manowari husika za kila upande.

Wizara hiyo imesema kwamba mazoezi hayo ni sehemu ya mpango wa ushirikiano wa kila mwaka kati ya majeshi hayo wawili na yanalenga kukabiliana kwa pamoja na changamoto za usalama na kulinda amani na utulivu wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha