Lugha Nyingine
Kampuni ya kuunda magari ya Chery ya China yafungua kiwanda cha kwanza Afrika Kusini, yalenga soko pana la Afrika (4)
![]() |
| Jamaa akipiga picha kwenye eneo la maonyesho la kiwanda cha kuzalisha magari cha Chery, Pretoria, Afrika Kusini, Julai 3, 2026. (Xinhua/Chen Wei) |
PRETORIA, Afrika Kusini - Kampuni ya kuunda magari ya Chery ya China imezindua rasmi kiwanda chake cha kuzalisha magari siku ya Ijumaa huko Rosslyn, kaskazini mwa mji mkuu wa utawala wa Afrika Kusini, Pretoria, ikiashiria mabadiliko yake ya kuwa mzalishaji magari wa nchini humo na kuzidisha dhamira yake ya muda mrefu kwa soko la Afrika Kusini.
Akihutubia hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho, Mwenyekiti wa Chery Yin Tongyue amesema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya muda mrefu ya kampuni hiyo kwa Afrika Kusini.
"Tumehama kutoka kuwa muagizaji hadi mzalishaji, na kutoka kuwa mshiriki wa soko hadi mshirika wa muda mrefu katika simulizi ya viwanda ya Afrika Kusini," amesema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu Rais wa Afrika Kusini, Paul Mashatile, amesema "Uwekezaji wa Chery utafungua njia ya uhamishaji teknolojia, otomesheni, mambo ya kidijitali na mifumo ya uzalishaji ya hali ya juu," akibainisha kuwa maendeleo hayo yataimarisha uwezo wa viwanda wa Afrika Kusini.
Pembeni mwa hafla hiyo, Mashatile ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini China, kampuni nyingi za China zilionyesha nia ya kuwekeza Afrika Kusini.
"Niliwaambia, 'Mnapokuja Afrika Kusini, mtapata fursa ya kupanuka katika bara la Afrika,'" amesema.
Balozi wa China nchini Afrika Kusini, Wu Peng, amesema kwamba safari mbili za aina yake zimekutana -- kiwanda cha Rosslyn, kiwanda cha kihistoria kinachowakilisha urithi wa tasnia ya magari ya Afrika Kusini, na Chery, muundaji magari wa China mwenye nguvu hai, wakiungana mkono ili kusonga mbele pamoja.
"Ushirikiano huu si tu kwamba unasimama kama ushuhuda dhahiri wa ushirikiano unaozidi kuongezeka kati ya China na Afrika Kusini, lakini pia utaingiza kasi mpya kwenye ushirikiano wetu wa pande mbili katika sekta ya magari na kufungua matarajio mapana zaidi kwa maendeleo ya siku za baadaye," Wu amesema.
Kwa mujibu wa Chery, uzalishaji katika kiwanda hicho cha Rosslyn umepangwa kuanza katikati ya mwaka 2027, huku uzalishaji wa awali wa magari 15,000 ukipangwa kuanza katika robo ya tatu na ya nne ya mwaka huo. Kwa uwezo kamili, kiwanda hico kinatarajiwa kuzalisha magari 50,000 kwa mwaka kwa zamu moja.
Kampuni hiyo imesema kwamba imedhamiria kubakisha wafanyakazi wote 692 waliopo wakati huohuo itazalisha ajira karibu 3,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika uzalishaji, minyororo ya usambazaji na huduma zinazohusiana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




