Bustani ya kitaifa ya eneo la mabaki ya kiakiolojia la Niuheliang nchini China yaonyesha urithi wa kitamaduni wa Hongshan (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2026
Bustani ya kitaifa ya eneo la mabaki ya kiakiolojia la Niuheliang nchini China yaonyesha urithi wa kitamaduni wa Hongshan
Picha iliyopigwa Agosti 4, 2026 ikionyesha ukumbi wa maonyesho ndani ya bustani ya kitaifa ya eneo la mabaki ya kiakiolojia la Niuheliang mjini Chaoyang, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Li Gang)

Bustani ya kitaifa ya eneo la mabaki ya kiakiolojia la Niuheliang katika Mji wa Chaoyang, Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China ilijengwa kwenye eneo la Niuheliang, eneo kubwa la kabla ya historia la ibada za matambiko na mazishi lenye hekalu la mungu wa kike, madhabahu na makaburi ya mawe.

Eneo hilo lenye historia ya zaidi ya miaka 5,000, liliibua zana za mawe, mabaki ya sanaa za udongo na jade zenye mapambo ya dragoni, phoenix na binadamu, ambazo zinaakisi mila na imani za utamaduni wa Hongshan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha