Lugha Nyingine
Roketi ya Changzheng 8A ya China iliyobeba satalaiti za intaneti za kikundi kipya yarushwa anga ya juu (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2026
![]() |
| Roketi ya uchukuzi ya Changzheng 8A iliyobeba satalaiti za intaneti za kikundi cha 23 za obiti ya chini ya anga ya juu, ikirushwa kutoka eneo la shughuli za kibiashara la kurushia vyombo vya anga ya juu la Wenchang, mkoani Hainan, kusini mwa China, Agosti 4, 2026. (Picha na Liu Jianqiu/Xinhua) |
WENCHANG - China imerusha satalaiti za intaneti za kikundi kipya kwenye obiti ya anga ya juu jana Jumanne kutoka eneo la shughuli za kibiashara la kurushia vyombo vya anga ya juu katika mkoa wa kisiwa wa Hainan, kusini mwa China.
Satalaiti hizo za intaneti za kikundi cha 23 za obiti ya chini, zimerushwa anga ya juu zikibebwa na roketi ya uchukuzi ya Changzheng 8A saa 10:52 ya jana jioni (Saa za Beijing) na kuingia kwenye obiti zao zilizopangwa mapema kwa mafanikio.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




