Lugha Nyingine
Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-21 waonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya jukumu la anga ya juu la siku 210 (2)
![]() |
| Mwanaanga wa chombo cha Shenzhou-21 Wu Fei akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, mji mkuu wa China, Agosti 5, 2026. (Picha na Zhang Wenjun/Xinhua) |
BEIJING - Wanaanga watatu kutoka jukumu la chombo cha Shenzhou-21 cha China wamekutana na waandishi wa habari mjini Beijing jana Jumatano, ikiwa ni kuonekana kwao kwa mara ya kwanza hadharani baada ya kurudi duniani mwezi Mei mwaka huu.
Wanaanga hao Zhang Lu, Wu Fei na Zhang Hongzhang wako katika hali nzuri ya kimwili na kiakili, huku nguvu za misuli, ukakamavu na utimamu wa moyo na mishipa kwa kiasi kikubwa vikiwa vimerejea katika viwango vya kabla ya kuruka, kama ilivyotangazwa kwenye mkutano huo. Imeelezwa kuwa, kwa sasa wameingia katika awamu ya uchunguzi wa kurejea katika hali ya kawaida na wataanza tena mazoezi ya kawaida baada ya tathmini ya mwisho ya afya.
Wanaanga hao wa Shenzhou-21 waliishi siku 210 kwenye obiti, kuanzia siku ya kurushwa kwa chombo chao Oktoba 31, 2025, hadi waliporejea Mei 29, 2026, wakiweka rekodi mpya kwa kundi la wanaanga kukaa kwa muda mrefu zaidi kwa mara moja kwenye anga ya juu miongoni mwa wanaanga wa China.
Wakati wa jukumu lao hilo, walikamilisha matembezi matatu ya anga ya juu na kufanya majaribio ya kina kuhusu sayansi ya anga ya juu, hasa kushuhudia na kushiriki katika operesheni ya kwanza-kabisa ya uokoaji wa dharura kwenye obiti katika historia ya mpango wa China wa kupeleka binadamu anga ya juu.
"Mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura wa mpango wa anga ya juu wa China ulihimili jaribio halisi katika jukumu letu," amesema Zhang Lu, kamanda wa jukumu hilo. "Kuanzia kushughulikia chombo cha anga ya juu kilichoathiriwa na vifusi vya anga ya juu, kurekebisha ratiba yetu kwenye obiti na kubadilisha vyombo vya kurudia duniani, hadi kutekeleza utuaji wa dharura, mfumo mzima ulifanya kazi vizuri ili kuhakikisha usalama wetu."
Wu Fei, ambaye hapo awali alichangia katika uundaji wa moduli ya msingi ya Tianhe na moduli ya maabara ya Wentian, amesema kuendesha vifaa ndani ya obiti ambavyo aliwahi kuvijaribu duniani kulimfanya ahisi kama kawaida.
Mtaalamu anayeshughulikia vilivyobebwa na chombo Zhang Hongzhang ameelezea mafanikio kadhaa ya kisayansi yaliyopatikana wakati wa jukumu hilo, ikiwemo kwa mara ya kwanza kwa China kupanda nyanya za cheri na ngano bila udongo, kufuga panya kwa mara ya kwanza katika mazingira yanayofungwa kwenye anga ya juu, na kuthibitisha teknolojia muhimu za matumizi bora ya spektrali na mbolea ya maji.
Zaidi ya ratiba yao ngumu ya utafiti, wanaanga hao walipanda aina zaidi ya kumi za mazao, yakiwemo ya ngano, alizeti, nyanya, viazi vitamu na mnanaa, ambayo si tu ilisaidia kuboresha mbinu za upandaji kwenye obiti lakini pia ilileta furaha katika maisha yao ya muda mrefu katika anga ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




