Lugha Nyingine
Daraja lililojengwa na kampuni ya China lazinduliwa nchini Cameroon (3)
YAOUNDE - Cameroon Jumatano wiki hii ilizindua Daraja la Mto Nyong ambalo limejengwa na Kampuni ya Uhandishi ya First Highway ya China (CFHEC) huko Malombo katika tarafa ya Nyong-et-Kelle ya Mkoa wa Kati, ambako mji mkuu Yaounde upo.
Daraja hilo lililozinduliwa na Waziri wa Ujenzi wa Umma wa Cameroon Emmanuel Nganou Djoumessi, lina urefu wa mita 160. Linavuka kwenye Mto Nyong na linaungwa mkono na barabara za kulifikia zenye urefu wa mita 960.
Akihutubia hafla ya uzinduzi wa daraja hilo Djoumessi amesema mradi huo, ambao ni kiungo muhimu cha ushirikiano wa miundombinu kati ya Cameroon na China, utaboresha kwa kiasi kikubwa muunganisho katika mkoa huo.
Amesema daraja hilo linachochea maendeleo ya kiuchumi kwa vijiji vinavyozunguka Mto Nyong.
"Mradi uliokabidhiwa leo tayari unaboresha mtiririko wa trafiki ndani ya mtandao wa usafiri wa Nyong-et-Kelle na njia za kwenda vituo vya utawala. Daraja hili linawakilisha mbali zaidi ya muundombinu wa kuvuka mto," waziri huyo amesema.
Yang Song, meneja mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Kimataifa cha CFHEC, ameliita daraja hilo kuwa ni ishara ya urafiki kati ya China na Cameroon.
"Daraja hili si tu njia ya trafiki inayounganisha pande mbili za Mto Nyong, bali pia ni daraja la urafiki na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili za China na Cameroon." Amesema.
Amesema kwa kutazama siku za baadaye, CFHEC itaendelea kushikilia moyo wa udhati na kunufaishana, kuongeza kwa kina ushirikiano wa kivitendo na Cameroon na kuwezesha maendeleo yenye sifa bora ya nchi hiyo kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na uzoefu mwingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




