Mfumuko wa bei wa Ghana wapungua hadi asilimia 4.6 mwezi Julai (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2026
Mfumuko wa bei wa Ghana wapungua hadi asilimia 4.6 mwezi Julai
Picha iliyopigwa Agosti 6, 2026 ikionyesha kituo cha petroli, Accra, Ghana. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Kiwango cha mfumuko wa bei wa mwaka wa Ghana kilishuka hadi asilimia 4.6 mwezi Julai kutoka asilimia 5.3 mwezi Juni, ikiwa ni kupungua kwa mara ya kwanza kwa mfumuko wa bei tangu Machi, Huduma ya Takwimu ya Ghana (GSS) imetangaza jana Alhamisi.

Mtakwimu wa Serikali ya Ghana Alhassan Iddrisu amesema kushuka huko kwa asilimia za pointi 0.7 kumetokana kwa kiasi kikubwa na kushuka kwa mfumuko wa bei wa bidhaa za chakula, ambao unabaki kuwa mchangiaji mkubwa zaidi wa mabadiliko katika fahirisi ya bei za walaji (CPI).

"Ikilinganishwa na asilimia 3.9 mwezi Juni, mfumuko wa bei wa bidhaa za chakula ulikuwa asilimia 3.1 mwezi Julai, wakati mfumuko wa bei usiotokana na bidhaa za chakula pia ulipungua hadi asilimia 6.1 mwezi Julai kutoka asilimia 6.3 mwezi uliopita," Iddrisu amesema.

Mfumuko wa bei wa bidhaa zinazozalishwa ndani ulipungua hadi asilimia 5.9 mwezi Julai kutoka asilimia 6.7 mwezi uliopita, wakati mfumuko wa bei wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ulishuka hadi asilimia 2 kutoka asilimia 2.3.

Mwezi uliopita, Benki Kuu ya Ghana ilidumisha kiwango chake cha kukopa bila kukikadilisha katika asilimia 14, ikirejelea hali zinazoendelea za kutokuwa na uhakika kwa siasa za kijiografia duniani.

Licha ya hatari za nje kwa matarajio ya mfumuko wa bei, Gavana wa Benki Kuu ya Ghana Johnson Asiama alisema Kamati ya Sera ya Fedha ya benki kuu hiyo imesema kwamba matarajio ya mfumuko wa bei na matarajio ya ya mfumuko wa bei wa msingi yalibaki kwa kiasi kikubwa ndani ya kiwango lengwa cha asilimia 6 hadi 10.

Asiama alisema kwamba hata mvurugiko wa muda mrefu wa usafirishaji kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao unaweza kuongeza bei ya mafuta ghafi duniani, haukuwa na uwezekano wa kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Ghana. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha