Treni ya kutoka Heilongjiang hadi Beijing yaandaliwa kwa ajili ya ziara ya masomo ya wanafunzi na walimu (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2026
Treni ya kutoka Heilongjiang hadi Beijing yaandaliwa kwa ajili ya ziara ya masomo ya wanafunzi na walimu
Mfanyakazi akiongoza wanafunzi kupanda treni maalum kwa ajili ya ziara ya masomo kwenye stesheni ya reli ya Qiqihar, Agosti 9, 2026. (Picha na Xu Shuai/Xinhua)

Treni maalum No. Y404 kwa ajili ya ziara ya masomo iliyobeba walimu na wanafunzi 598 jana Jumapili iliondoka kutoka stesheni ya reli ya Qiqihar katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China kuelekea Beijing, mji mkuu wa China.

Treni hiyo ya kutoka Heilongjiang hadi Beijing imeandaliwa na Kampuni ya Kundi la Harbin la Shirika la Reli la China mwaka huu kwa ajili ya wanafunzi wanaofanya ziara za masomo, ikitumika kama darasa linalohamahama, ambapo shughuli za kuimba na kucheza ngoma zinafanyika ndani ya treni, na wanafunzi wanapokuwa njiani wanapata nafasi ya kuchangamana na kufurahia mvuto wa utamaduni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha