Lugha Nyingine
Kimbunga Pomboo chatua Zhejiang kwenye pwani ya mashariki ya China
HANGZHOU - Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa cha China (NMC) kimesema, Kimbunga Pomboo ambacho ni kimbunga cha 13 kwa mwaka huu kuikumba China, kilitua mjini Yuhuan huko Taizhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, majira ya saa 11:30 jioni jana Jumapili.
Kituo hicho kimesema, upepo mkali zaidi uliodumu karibu na kiini cha kimbunga hicho nguvu yake ilifikia daraja la 14, au mita 42 kwa sekunde, na kukifanya kimbunga Pomboo kuwa kimbunga kikali zaidi wakati kilipotua.
Kituo cha hali ya hewa kimetoa tahadhari kwa mamlaka za serikali za mitaa katika maeneo yaliyoathiriwa kujilinda wakati mvua kubwa uliponyesha kwa kuzidi kiasi.
Mapema siku hiyo ya Jumapili Kituo cha hali ya hewa cha kitaifa kilitoa tahadhari nyekundu – ngazi ya juu zaidi katika mfumo wa tahadhari ya kimbunga wa China – wakati ambapo Kimbunga Pomboo kilikuwa kimekaribia.
Kimekadiria kuwa, kuanzia Jumapili iliyopita hadi Jumatano wiki hii, kimbunga hicho kitaleta mvua kubwa sana katika maeneo mbalimbali katika mikoa ya Fujian na Zhejiang na mji wa Shanghai, na pia kitaathiri mkoa wa Shandong, miji ya Tianjin na Beijing. Maeneo hayo yatakayoathiriwa pia yatapata mvua kubwa ya muda-mfupi na dhoruba za radi pamoja na upepo wa nguvu ya dhoruba.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




