Lugha Nyingine
Msimu wa 2 wa onyesho la vipaji la "Imba kwa Afrika" linaloungwa mkono na China wazinduliwa nchini Kenya
![]() |
| Mwimbaji akitumbuiza kwenye hafla ya msimu wa pili wa onyesho la vipaji vya muziki "Imba kwa Afrika" jijini Nairobi, Kenya, Agosti 7, 2026. (Xinhua/Yang Guang) |
NAIROBI – Msimu wa pili wa onyesho la vipaji vya muziki linaloungwa mkono na China la "Imba kwa Afrika" umezinduliwa Ijumaa jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa waandamizi, wanadiplomasia, watendaji wa tasnia, wasomi na wasanii chipukizi.
“Imba kwa Afrika” ambayo ni programu kuu ya Mwaka 2026 wa Mabadilishano ya kati ya Watu wa China na Afrika, inalenga kukuza vipaji vya muziki vya ndani ya Afrika wakati huohuo ikitengeneza jukwaa la kuhimiza mazungumzo ya kuvuka-tamaduni.
Msimu huo wa pili wa onyesho hilo la vipaji vya muziki utashirikisha safu ya wanawake pekee, ukijenga juu ya mafanikio ya msimu wa kwanza ambao ulishirikisha washindani wa kiume pekee na ulioanza Novemba 2025 hadi Februari mwaka huu.
Kwa mujibu wa waandaaji, Msimu wa 2 wa "Imba kwa Afrika" utaanza na maonyesho ya kuchuja washiriki katika taasisi za elimu ya juu na katika mitaa ya mijini, na kupunguza washiriki hadi 21 watakaojiunga na akademi kwa ajili ya unasihi kutoka kwa watu mashuhuri wa tasnia ya burudani.
Anne Wang'ombe, katibu mkuu wa Idara ya Jinsia na Hatua za Kutetea Usawa wa Kijamii katika Wizara ya Jinsia, Utamaduni na Huduma za Watoto ya Kenya, amesema onyesho hilo la vipaji litaongeza kwa kina mazungumzo ya kitamaduni, urafiki, kuaminiana na kuheshimiana kati ya China na Afrika.
"Muziki tunaouzindua leo unaashiria mapatano, umoja na ustawi wa pamoja kati ya watu wa Afrika na China," amesema Wang'ombe, akiongeza kuwa kukuza vipaji vya ubunifu ni muhimu katika kuharakisha mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi barani Afrika.
Zhang Zhizhong, waziri mshauri katika Ubalozi wa China nchini Kenya, amesema muziki ni lugha ya watu wote duniani inayovuka mipaka ya kitaifa, inayoweza kuwasiliana na moyo na ni jukwaa muhimu la kuhimiza kufunzana miongoni mwa ustaarabu mbalimbali.
Kwa mujibu wa Zhang, Msimu huo wa 2 wa "Imba kwa Afrika" utatoa jukwaa kwa wanamuziki wa kike kutoka barani Afrika kuonyesha vipaji vyao na kutimiza ndoto zao, ukijenga juu ya mafanikio ya Msimu wa 1, ambao ulijikita katika shauku na ndoto za wanamuziki wa kiume kutoka bara hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




